Jinsi ya kupata matokeo makubwa;kwa kila unachofanya.

Kanuni hii imewasaidia watu wengi sana katika mabo yao kufikia mafanikio makubwa;kanuni hii inaitwa The lawa of 40% kwa mara ya kwanza ilisemwa na jesse izras
katika kitabu chake cha ""
ambapo alimtafuta mtu mmoja ambaye alikuwa amepitia katika jeshi la marekani na alikuwa mashuhuri katika masuala ya physical fitness.
akamwambia naomba unisaidie kuandaa programu ya mazoezi.
sasa yule jamaa alipoanza programu akaanza kumfanyisha push up,na alipomfanyia push up,mzee jesse anamwambia mimi hiyo siwezi kufanya
yeye anamwambia pumzika tutaendelea.
anapumzika dakika chache anamrudisha tena.Baadae akaja kugundua kwamba kila alipofanya zile push up uwezo wake ulikuwa ni 40% tu.bado kulikuwa na uwezekano wa 60% yeye kuendelea kufanya.
2018mkuna tafiti zilifanyika na zikaonesha kila wakati unapohisi umefika mwisho huwezi kuendelea,umetumia uwezo wote;ukifika hatua hiyo umetumia 40% tu ya kile unachoweza kufanya bado kuna 60% unaweza kuifanya.
Kila inapokuja hiyo hali jisemee no! no! no! 40% tu hazitoshi.

kanuni hii unaweza kuitumia kwenye kazi yako,kwenye mahusiano,kwenye biashara na kwingineko.
una uwezo mkubwa kuliko unavyojiona.
katika kila hatua unapofikia ukazani inatosha ujue hiyo ni 40% ya kile unatakiwa kukifanya.
KILA MWANADAMU ANA RESERVE Tank,kama gari mafuta yakiisha kwenye tank la kwanza kuna mafuta ya akiba tank la pili.
Unao uwezo wa kuvumilia na kufanya kitu cha ziada.

Jiulize katika kitu ninachokifanya nawezaje kuitumia reserve tank yangu?
Inawezekana unahisi umefika mwisho kabisa,katika kazi zako,katika mahusiano yako unahisi huwezi tena kuendelea.
kanuni hii inasema hayo yote uliyoyafanya mara ya kwanza ni 40% tu;unaweza kufanya zaidi kwa 60% tena na usipate shida yoyote.

60% zilizobaki ni nyingi kuliko tulizofanya,kwa nini tusianze kuzifikia katika mambo yetu tunayofanya?
Niandikie hapo chini;kitu gani ambacho utakifanya kuanzia sasa ili kufanya ufike pale unapaswa kufika kwa kufanya zaidi ya ulivyokuwa unafanya.
Fikira angavu;mapambazuko ya washindi.

Chapisha Maoni

0 Maoni