KWA NINI NI MUHIMU KUGUNDUA KUSU LAKO LA MAISHA?

Tunapaswa kutambua kusudi la kuwepo duniani na kuliishi.
Kwa nini ni muhimu kugundua kusudi la maisha? ni madhara gani yanatokea ikiwa hutagundua kusudi la maisha?

MUHIMU: Ukigundua kusudi lako la maisha utaanza kupata mwelekeo wa maisha yako.
wengi wanaamka asubuhi wanakwenda kazini,wanakwenda kwenye biashara,wanafanya vitu mbalimbali,lakini ukiwauliza swali la unakusudia kupata jambo gani?
baada ya miaka kumi utakuwa wapi? watu wengi hawawezi kujibu swali hilo.

Unapoishi nje ya kusudi huna tofauti na kiumbe aliyeumbwa kuishi mahali fulani ila kikaamua kuishi mahali kwingine.

MFANO:Samaki ukimutoa nje ya maji,hahuhitaji kumuua maana hadi hapo muda ukifika tu atakufa.

wengi wameshindwa kufanikiwa kwa sababu wanaishi nje ya kusudi lao la maisha,na hiyo ndiyo sababu ya maisha yao magumu.
 ukiishi nje ya kusudi lako la maisha utakosa hamasa kwa hiyo utakuwa na upungufu wa nguvu.

JIULIZE:Katika kile unacho kifanya una hamasa kiasi gani? je unafanya kama umelazimishwa? unapokwenda kazini unakuwa na mkali ya kazi?

Taasisi ya moyo ya marekani walifanya utafiti wakagundua; watu wengi sana wenye matatizo ya moyo wanakufa sana siku ya Jumatatu saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.
walipoingia ndani kugundua chanzo walibaini kuwa;baada ya kazi watu walifurahia weekend,na vitu wanavyopenda kuvifanya;lakini sasa jumatau wanapaswa kwenda kazini,kwenye kazi wasizopenda kufanya
na wanakwenda kufanya vitu ambavyo havikuwa ndoto zao kabisa.

Je kitu unachokifanya unakifurahia kwa kiasi gani? je kuna namna unajuta? kuna wengi ambao wanafanya vitu ambavyo hawavipendi kabisa.Ila ni mazingira yamewalazimisha;pengine ilikuwa ni kozi pekee uliyofaulu vizuri.
Pengine ulipotafuta kazi ulikoswa kabisa ukapata hiyo unayofanya sasa hivi,lakini jambo ambalo ningependa kukuhakikishia katika maisha kama hufanyo jambo unalolipenda utakosa hamasa na hivyo kuwa na hali ngumu:ishi nda ya makusudi.

1.Je ninachokifanya ndicho nilichokuwa nikikitamani siku zote kukifanya katika maisha? au ningependa kufanya kitu kingine?

2.Je ninajihisi kufurahia,au najihisi nimekosa kitu nilichotaka kukifanya?
3.Je nipo tayari kubadilisha ninachokifanya nifanye kitu kingine?.

Kama umepata majibu ya maswali hayo unaweza kufika pale unapohitaji.
Niandikie chochote tutajadiliana kwa kina zaidi.ASANTE!

Chapisha Maoni

0 Maoni