NJIA 5 BORA ZA KULINDA NDOTO YAKO.

NJIA TANO ZA KUILINDA NDOTO YAKO.
je kuna ndoto yoyote ambayo unapenda kuitimiza katika maisha pengine hautaki mwaka huu uishe,bila kutimiza ndoto yako.
Na mapema kabla hujaondoka duniani uwe tayari umeshatimiza?
Unachotakiwa kujua tu ,ni kwamba;ndoto huwa inazaliwa,inakufa,pengine isife ila ikadumaa,lakini fahamu pia kuna ndoto huwa zinaishia njiani.
Kuna namna unaweza kufanya ili ndoto yako isife,wala isiishie njiani bali ukafikia mafanikio kabisa.

Hizi hapa ni njia tano zitakazofanya ndoto yako kufikia mafanikio na kisha ukaifurahia.
1.Kila siku fanya kitu kuhusiana na ndoto yako.
JOHN MAXWELL   "The secret of your success is in your daily duties" siri ya mafanikio yako iko katika kile unachokifanya kila siku.
Ni muhimu sana kujua kuwa siku yako ndiyo imebeba mafanikio ya wiki yako,na wiki yako imebeba mafanikio ya mwezi wako,na mwezi mafanikio ya mwaka kadhalika,mwaka umebeba mafanikio ya maisha yako.
maisha yako yamebebwa katika unavyotumia siku yako.

watu wengi wakiwa na ndoto huwa hawajali wanasema nitaanza kesho,nitafanya hiki;Hapana kila siku fanya kitu kuhusiana na ndoto yako ;hata kama ni kidogo sana,hata kama ni kusoma tu,hata kama ni kuandika,hata kama ni kuuliza ,hata kama ni kutafuta kitu fulani;fanya na fanya na fanya zaidi.

unapofanya kitu katika ndoto yako inakuwa hai na haitakufa,lakini ukichelea chelea! ndoto inakufa kabisa.na ndoto ikifa maana yake hakuna kufanikiwa tena.

Je! wewe leo umefanya kitu fulani kuhusu ndoto yako?



2.Pata mtu wa kuongea nae kila wakati kuhusu ndoto yako(accountability partner).
pata mtu ambaye kila wakati utamwambia umefanya nini,unafanya nini na unatarajia kufanya nini?
Hii itakufanya uwe makini kila wakati kwa mashauri yake na njia mpya za kuboresha unazopata.
kama ndoto unayo wewe tu hakuna anaye kuuliza,hutakuwa na hamasa zaidi ya kupambana.

MUHIMU:Mtu fulani kila wakati akiwa anazungumzia kuhusu jambo lako kuna namna ya kuhisi unatakiwa kufanya zaidi ya ulivyofanya tayari.


3.Tengeneza tabia zinazoendana na ndoto yako.(Intentional habits developments).
Kuna watu wengi ambao tayari ndoto zao wanazijua,na nini cha kufanya wanajua sana lakini tatizo ni kwamba kuna tabia zinazozuia wao kwenda mbele.
Tabia za kuacha:ukiendelea kuwa nazo utaendelea kufeli kila wakati.
Tabia za kuanza upya: Kwa lengo la kuongeza kasi ya kufikia ndoto.
Tabia za kupunguza: Hizi ni zile zina umuhimu fulani,na wakati huo zinapishana na ndoto yako(kuwa na kiasi)
Tabia za kuongeza: hizi unatakiwa kuzifanya zaidi ili uwe thabiti katika ndoto yako.kwa namna fulani tayari unafanya ila unatakiwa kuziongeza zaidi.
Kwa hiyo ni muhimu sana kujihoji,mambo gani ufanye zaidi na mambo gani uache zaidi ili ufanikiwe.
MFANO:Wanamichezo wana nidhamu za tabia katika vyakula,vinywaji na vitu vingine ili wabaki kuwa na nguvu sitahiki za mchezo.

kila siku punguza tabia fulani au ongeza tabia fulani ili uweze kufanikiwa.



4.Pata muda wa kufikiria kwa kina kuhusu ndoto yako(Imaginative thinking).
jaribu kupata picha kamili itakuwaje ikiwa ndoto yako itatimia,je itakuwaje ikiwa haitatimia,mambo gani unayahitaji zaidi kuifanya ndoto yako kuwa Bora,
je ni watu gani unawahitaji kushirikiana nao?
MUHIMU:Usipotoa muda kwa akili yako kutafakari utakosa hamasa ya kutenda zaidi.kwa sababu ili ndoto yako ifanikiwe inatakiwa iingie kwenye ubongo wa ndani zaidi wa akili yako(subconcious mind)
Kwa hiyo kila unapopata muda wa kutafakari,unaihamisha ndoto kutoka mawazo ya kawaida kuwa kitu unachokifanyia kazi.

4.Usijilinganishe na watu wengine.(Don't compare your number one chapter with others).
Tunaruhusiwa kujifunza kwa wengine ila siyo kuiga maisha yao.Kama mwenzako yupo ukurasa wa mia moja (100) usikupe shida kuwepo ukurasa wa kwanza(1).Maana kuna wakati yeye pia alikuwa ukurasa wa kwanza.
Ukiishi kwa kuwaigan watu inaweza kukukatisha tamaa sana na kuhisi wewe ni duni kumbe siyo kweli.Kila wakati lenga kwenye ndoto yako,kisha ijenge bila kukatishwa tamaa.
KUMBUKA:Hakuna wakati katika maisha yako,utakosa wa kukuzidi;la! lazima pawepo mtu juu yako,lazima pawe na mtu chini yako.Lazima pawe na mtu mbele yako, lazima pawe na mtu nyuma yako.
usikatishwe tamaa.

Katika vitu hivi vyote kitu gani kinaweza kukusaidia sana wewe kuilinda ndoto yako? Andika hapo chini kwenye comment! sisi ni jamii.


Chapisha Maoni

0 Maoni