Tambua kusudi la maisha yako.

Nitajuaje kusudi la maisha yangu? pengine hili ndilo swali ambalo limekutesa kwa muda mrefu.
leo tutajifunza namna ya kugundua kusudi la maisha yako.

1.angalia uwezo ulio nao.
ukweli ni kwamba kitu chochote kilichoumbwa duniani,kina kusudi la kuumbwa.
katika taratibu za uumbaji tunasema;kusudi lilitangulia uumbaji.(Purpose came first before creation)
kabla hujaja duniani palikuwa na kusudi lililowekwa kwanza ili kwamba utatue hilo tatizo,au utimize hilo kusudi.
Hakuna hata mmoja aliyepo duniani kwa bahati mbaya;lipo kusudi kwa nini unaishi.
Hata kama leo huyafurahii maisha yako,tambua lipo kusudi.
MUHIMU:Angalia upekee wako ,angalia nguvu yako,angalia jambo ambalo unalifanya vizuri bila kutumia nguvu kuliko watu wengine.

MIFANO:
1.Ndege anapozaliwa hahitaji kuchomwa sindano ili aweze kupaa angani
2.Samaki anapototolewa kwenye maji pia hahitaji kufundishwa kuogelea ili aogelee.

Wote hao wanafanya vema tu;kwa sababu uwezo wa kufanya hivyo wameumbwa nao;umo ndani yao.

na wewe ndani yako kuna uwezo wa kupekee; kama ukiugundua unaweza kukusaidia.

JIULIZE: Hivi kuna jambo gani ambalo nalifanya kwa urahisi zaidi kuliko mambo mengine?
Liandike jambo hilo kisha ;anza kulifanyia kazi,ghafla utapata urahisi zaidi wa kutimiza kusudi la wewe kuishi.

2.Angalia maisha yako ya nyuma.
jaribu kuangalia kuwa katika wakati gani wa maisha yako ulifikia mafanikio ya kiwango cha juu sana?
JIULIZE: Ni njia gani au jambo gani nililifanya kufikia hapo? kisha reja fanya tena kwa juhudi.
Ili mradi ni jambo sahihi huvunji sheria,utafanikiwa sana.


3.Waulize watu wako wa karibu;kuna kitu gani wanakiona ndani yako ambacho ni cha pekee sana?
wewe kama umeumbwa kuwa mwimbaji mkubwa,kuwa mchezaji wa mpira,kuwa mbunifu wa vitu;Tambua hilo jambo lipo chini ya uwezo wako.
Tatizo kubwa la watu;hawajitathimini,hawajiangalii,hawajikagui.

leo jaribu kufanya zoezi hilo;jiulize maswali matatu,ili ujue jinsi ambavyo maisha yako yanaweza kuwa yenye mafanikio zaidi.

Andika kwenye comment;kama tayari kuna kitu umekiona na tayari inakupasa ukilete kwenye maisha yako.ASANTE!

Chapisha Maoni

0 Maoni