Mambo 7:Unayotakiwa kuyaacha mwaka 2020

katika sayansi ya mafanikio kuna vitu 4 ambavyo lazima uvielewe ili kufanya viwango vya maisha yako vibadilike.
1.kuna mambo ambayo huyafanyi unatakiwa uanze kuyafanya.
2.kuna mambo unayo fanya ongeza kasi ya kuyafanya.
3.kuna mambo ambayo unafanya unatakiwa upunguze unavyo yafanya.
4.kuna mambo ambayo unatakiwa uache kabisa kuyafanya.

katika kufuatilia watu waliofanikiwa nimegundua kuwa kuna mambo 7 ambayo ni muhimu kuyaepuka ili kufanikiwa.
Lolote kati ya mambo haya saba, kama hutaweza kuliacha linatosha kabisa kukukwamisha kufikia malengo yako.

1.Hali ya kusubiri mtu aje kukusaidia(waiting for help).

 Kuna watu hawajaanza biashara kwa sababu kuna mtu wanamsubiri
aliahidi atawapa mtaji sasa ni mwaka wa tatu.wengine hawajapata kazi kwa sababu kuna mtu aliwaahidi kuwa, anawatafutia kazi.
kama ukiwa mtu wa aina hii kwa kweli itakukatisha tamaa sana, na kukwamisha kufikia malengo yako.na kutofika kule unakotaka kwenda.
ili ufanikiwe chukua 100% ya wajibu wa maisha yako.kama unasubiri mtu wa kukusaidia hakika hakika hutafika unakokwenda. koma kusubiri watu.
chukua maisha kama wajibu wako na anza hatua leo.

2.Kulalamika.(Complaint)

Watu wengi ambao wamefanikiwa, wamejitahidi sana kuishinda hii hali.
Watu wengi wameshindwa kuendelea,wameshindwa kutimiza ndoto,wameshindwa kupiga hatua kwa sababu ya kulalamika.
Ukiwa mtu wa malalamiko kuna watu unawafukuza katika maisha yako.
Pengine umekuwa na rafiki wa malalamiko,ukimtembelea analalamika,ukimpigia simu analalamika,kila unachofanya analalamika,Huwezi kufurahia kuwa na rafiki wa namna hii.

kila fursa kwenye maisha yako huletwa na watu kwa hiyo watu wakikukimbia na fursa nazo zinaondoka.
Kuna watu wanalalamika tangu mapambazuko hadi wanakwenda kulala,hiyo mbaya sana.

MUHIMU:Jitahidi kujikataza kulalamika kila unapopata sababu ya kulalamika.siyo kitu rahisi lakini jifunze kuona kitu chema katika kila kitu kibaya.(learn to see postive in every negative things)

Katika hilo lililo kutokea kuna kitu chema unaweza kujifunza?

3.Kuacha kusubiri maajabu(waiting for one breakthrough)

Watu wanaishi kana kwamba, wanasubiri kushinda bahati nasibu,kwamba kufumba na kufumbua kitu kitatokea na maisha yatabadilika,usiku mmoja(overnight) .lazima ukubali kufanya kazi hatua moja baada ya nyingine.watu wanaofanikiwa wameacha kusubiri mpenyo mmoja tu wa kubadili maisha yao.wanachofanya kila siku wanafanya kitu kuelekea katika ndoto walizonazo.

4.Kutokuendana kati ya maneno na matendo(inconsistence btn your words and action)

Watu wengi mwaka unapoanza,au wanapohudhuria semina,au wamepata hamasa fulani,kitu cha kwanza wataanza kuzungumza; mimi nataka kufanya hiki,nataka kubadilisha hiki,kuwa mtunza muda mzuri,nataka kutimiza malengo yangu N.k;lakini bado wanaendelea vilevile.

MUHIMU:Maisha hayabadilishi na kile unachokisema bali maisha yanabadilishwa na kile unachokifanya.

Ndiyo maana kuna watu wengi wanajua vitu vingi na wanazungumza vitu vingi ila maisha yao yako vilevile.
Ili ufanikiwe unachokijua lazima kionekane kwa vitendo.
jiulize,mambo gani umekuwa ukisema sana lakini hujawahi kuyafanyia kazi?
acha kabisa kuwa mtu ambaye maneno yako na matendo yako haviendani.

5.kukaa katika makosa ya nyuma .(dweling on your past mistake)

Kuna watu wameshindwa kufanikiwa; kwa sababu ya kuishi katika makosa ya nyuma,walifeli mtihani,walifukuzwa shule,walishindwa katika biashara,walishindwa katika mahusiano.kwa hiyo kila wakikumbuka wanahisi hawawezi,wanashindwa kupiga hatua na kusonga mbele ili kufikia mafanikio yao.
Kila mtu anafanya makosa,lakini tofauti ya watu wawili wanaokosea siyo kiwango cha kosa lao ila jambo gani watafanya baada ya kukosea?
wengine wanainuka ,wanasahihisha na kuendelea na safari,wengine wanalia,wanalalamika,watasimulia mwaka huu watasimulia mwaka kesho vile ambavyo jambo lile limewakwamisha sana.
kila mwaka anasimulia kitu kilekile.kila wakati anakaa katika makosa yake.
acha kabisa kuishi kwenye makosa.
ni kweli kuna watu watayatumia makosa yako kama fimbo lakini,usiishi katika makosa ya nyuma.fanya masahihisho kisha endelea mbele.
Fungua ukurasa mpya wa maisha yako.kuna wengi wamefanya makosa lakini leo wanaishi maisha mazuri kabisa.

6.Kuacha kujihisi kuwa Muhanga(Feeling a victim)

Kuna watu wanahisi kuwa; wahanga wa matatizo kana kwamba wao ndio walioumbiwa matatizo,hali hiyo itakuzuia kwenda mbele.
Baba alikukataa,sawa lakini usiwe muhanga wa hilo tatizo.
ukiwa unajihisi muhanga utaanza kujidharau,utapoteza kujiamini(inferiority complex).
acha kujiona kama muhanga,ongeza thamani ya maisha yako,mapya mapya yataanza kutokea.

7.Kuacha kutokufanya maamuzi.

Kuna watu wanakawia kufanya maamuzi,kwa hiyo baadae akifanya maamuzi yanakuwa hayana thamani kabisa.
lakini pia kuna watu ambao hawafanyi kabisa maamuzi wao wanajua,mambo yatatokea tu yenyewe,siyo kweli.Hapo ulipo leo ni matokea ya maamuzi yaliyofanyika jana
na kule utakako kuwa kesho ni matokea ya kile utakacho amua leo.
kuna maamuzi unatakiwa uyafanye kuhusiana na mahusiano yako,kazi yako,biashara yako.

KUMBUKA:Kuna maamuzi ukiyafanya yatakupa maumivu,lakini yatakuwa ya muda mfupi tu.usiache kufanya maamuzi.


Kuna maamuzi ukiyafanya watu hawatakuelewa kabisa.Lakini kumbuka kuwa hakuna anayewajibika kukuamulia maisha ,hata kama kila mtu hakuelewi; lakini wewe unajua kabisa utapata faida;fanya.
Kuna maamuzi yamefungwa katika muda,usipofanya hayarudi nyuma.Fanya maamuzi thabiti kuhusu maisha yako ufike unakotaka kwenda.

Tuandikie hapo chini;kwenye comment:

 Kama kuna jambo unalotaka kuliacha mara moja lakini unahisi ni vigumu sana,ili tusaidiane kufikia maisha bora na yenye mafanikio.ASANTE!


Chapisha Maoni

0 Maoni